Katika hali ya kawaida, sio rahisi kuona maji yanayotoka kwenye mfumo wa Exhaust wa gari. Lakini ukigundua kuwa bomba lako la nyuma linavuja au linadondosha maji kutoka humo, basi ina maana kwamba mfumo wako wa kutolea moshi lazima uwe na maji ndani yake.
Hii sio sababu ya kuwa na wasiwasi sana kwa sababu kwa kawaida hali hii sio jambo kubwa. Hata hivyo, imekuwa ni jambo zuri kufanya uchunguzi wa hali hii na ukatenga muda kusoma nakala hii. Vinginevyo, inaweza kuunda matokeo mabaya zaidi ambayo yatakugharimu pesa nyingi kama usipojua tatizo nini.
zifuatazo ni baadhi ya sababu Kwanini Gari hutoa Maji kwenye Exhaust.
moja ya viashiria kua injini yako ipo vizuri hasa katika utendaji wake wa kazi ni kuona maji yanatoka kwenye Exhaust ingawa sio magari yote yanayotoa maji basi inaashiria hivi lakini magari mengi. Injini yako inapo unguza mafuta iwe petrol au diesel kinachofuata kama matokeo niĀ Gas aina ya Kaboni dioksidi na maji. hii pia husaidia kupunguza kiwango cha hewa chafu kitakachotelewa na gari yako.
Pia sababu nyingine ya Gari kutoa maji kwenye Exhaust, kama unaishi kwenye maeneo yenye baridi kama Iringa, mbeya arusha na singida basi vitu kama hivi ni rahisi kuona kwani injini yako inapopata joto ile hewa ya baridi inayo ingia kwenye Exhaust. Kwa sababu hii, mvuke wa maji hutolewa wakati joto linapounganishwa na hewa baridi. Kisha utaona matone madogo ya maji yakianguka kutoka kwenye bomba la nyuma pamoja na kile kinachoonekana kuwa moshi mweupe. hata hivyo hali hii hutoweka baada ya muda mchache tu.
sababu nyingine ambayo husababisha maji kutoka kwenye mfumo wa kutolea hewa chafu yani Exhaust ni ubovu wa piston ya gari yako. lakini hii hua ina viashiria vyake kutambua kwamba kuna kitu hakipo sawa utaona vitu vifuatavyo.
Exhaust yako inatoa maji pamoja na moshi muda huo, ikiambatana na harufu isiyo ya kawaida, na maranyingi harufu hii hua ni nzuri na yenye kuvutia.
utakapo ona hali hii haraka sana usiendeshe gari yako na muite fundi wa mechanic aje akague piston yako kuthibitisha uwepo wa tatizo hilo.
Tuuzie Gari yako tembelea: magaribeipoa.com
Comments