Kama ilivyo kwetu sisi binadamu hatujakamilika basi hata kipimo cha mimba nacho haikiwezi kua sahihi muda wote. Kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kusababisha kipimo cha mimba kutoa matokeo yasiyo sahihi ambazo ni.
Kupima mapema sana: Kipimo cha mimba kinahitaji kuwepo kwa kiwango cha kutosha cha homoni ya chorionic gonadotropin (hCG) ambayo hujulikana kama homoni ya ujauzito. Ikiwa mtu anapima kabla ya muda wa mimba kuongezeka hivyo homoni ya hCG inaweza kuwa haijaongezeka vya kutosha na kipimo kikaonyesha matokeo hasi (negative) hata kama mimba ipo.
Kutumia kipimo kilichoisha muda wake: Kipimo cha mimba kinaweza kudanganya ikiwa kilitumika baada ya muda wake wa matumizi kuisha.
Vipimo visivyo sahihi: Baadhi ya vipimo vya mimba visivyoaminika havina uwezo wa kugundua mimba mapema au hutoa matokeo ya uwongo.
Mimba ya ectopic: Mimba ya ectopic hutokea wakati mimba inashikiliwa nje ya mfuko wa uzazi. Katika hali hii, kiwango cha hCG kinaweza kuwa kidogo sana, ambacho kinaweza kusababisha kipimo cha mimba kutoa matokeo hasi wakati kuna mimba.
Mimba ambayo imekoma: Mimba iliyokomaa inaweza kuwa na kiwango cha chini cha hCG ambacho hakiwezi kugunduliwa na kipimo cha mimba.
Kwa hivyo, ni muhimu kuzingatia matokeo ya vipimo vya mimba kwa uangalifu na ikiwa kuna mashaka yoyote, ni vyema kufanya vipimo zaidi au kushauriana na daktari.
Comments