Epuka usumbufu tembelea mfumo wa tausi tamisemi kupata leseni yako ya biashara yako kwa haraka.
Hakikisha kabla ya kuomba leseni ya biashara basi una TIN number, yani Utambulisho wa Mlipakodi na baada ya hapo mwombaji atatakiwa kuomba leseni ya biashara kutoka ofisi za Biashara katika Wilaya, Manispaa, Jiji na Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kutegemea na aina ya biashara anayotaka kuanzisha.
Aina za biashara watoaji wa leseni wamezigawa katika makundi mawili nayo ni Kundi A na kundi B
Mfano wa Biashara zilizo kwenye Kundi B:
Kwa biashara ya kundi A zinazo jumuisha viwanda vikubwa vinavyo ajiri watu wengi, mtaji mkubwa na pia hata eneo inalochukua inakua ni kubwa kiasi Leseni za Kundi A hutolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara.
soma pia:-
Kwanza uta Download fomu ya maombi ya leseni ya biashara, na baada ya hapo utajaza taarifa zako kama jina lako na utaambatanisha:-
Kwa leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali, Kwa mfano (TFDA, EWURA, TAURA, CRB, TILLI) n.k lazima mwombaji kuwa na leseni husika kabla ya kuomba leseni ya biashara fomu ya maombi ya biashara (TFN 211) hutolewa kwa ada ya Tshs. 1,000/=.
NB: Leseni hii huisha muda wake mwaka mmoja (1) tangu tarehe ilipoanza kutumika.
Baada ya kujaza fomu na viambatanisho, maombi hupitishwa ngazi zinazotakiwa kisheria – Mpango Miji na Afya. Baada ya hapo leseni hutolewa ndani ya siku moja au mbili na si zaidi.
Kusajili biashara ina faida kadhaa muhimu. Hapa chini ni baadhi ya faida za kusajili biashara:
Uhalali na Uaminifu: Kusajili biashara kunatoa hali ya uhalali na uaminifu kwa biashara yako. Inaonyesha kuwa biashara yako ni halali na imezingatia sheria na kanuni zinazohusiana na biashara hiyo.
Ulinzi wa Jina la Biashara: Kusajili biashara kunakupa haki ya kipekee na ulinzi wa jina la biashara yako. Hii inamaanisha kuwa hakuna mtu mwingine anayeweza kutumia jina lile lile au jina linalofanana na biashara yako katika eneo la kijiografia lililosajiliwa.
Kupata Mikopo na Uwekezaji: Benki na taasisi nyingine za fedha mara nyingi zinahitaji usajili wa biashara kabla ya kutoa mikopo au ufadhili. Kwa kuwa umesajili biashara yako, inakuwa rahisi kupata mikopo na uwekezaji kutoka vyanzo mbalimbali.
Upatikanaji wa Soko: Kusajili biashara kunakupa fursa ya kufanya biashara na taasisi za umma, makampuni, au wateja wengine ambao wanahitaji ushahidi wa uhalali wa biashara unayofanya nao biashara.
Ulinzi wa Mali na Dhima: Kusajili biashara kama kampuni inaweza kukupa ulinzi wa kibinafsi. Ikiwa biashara yako itashindwa au kukabiliwa na masuala ya kisheria, unaweza kuwa na kinga ya kibinafsi dhidi ya madeni ya biashara na hatari ya kupoteza mali yako binafsi.
Ukuaji na Mafanikio: Kusajili biashara kunaweza kusaidia kujenga msingi imara wa ukuaji wa biashara. Inakupa fursa ya kushiriki katika zabuni za serikali, ushirikiano na makampuni mengine, na kuongeza sifa yako kama mtoa huduma au muuzaji.
Ni muhimu kukumbuka kuwa leseni ya biashara ni hati ya kuthibitisha uhalali wa kufanya biashara kisheria. Ni jukumu la mmiliki wa leseni kuhakikisha kuwa anafuata sheria na kufanya biashara kwa usalama wake na watumiaji wa bidhaa zake wakati wote.
Comments