kama leseni yako imeisha muda wake au imepotea utahitaji kurenew au kwa kiswahili fasaha tunasema kuibadilisha. Mchakato ni rahisi, lakini kuna mambo machache ambayo unahitaji kufanya ili kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda sawa.
soma pia: Bei ya leseni ya udereva
Makala hii itakupa mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kubadilisha leseni ya udereva nchini Tanzania (Jinsi Ya Kurenew Leseni ya Udereva 2023 Online). Fuata maagizo kwa uangalifu na utaweza kupata leseni yako mpya.
Kubadilisha leseni ya udereva daraja zote Fuata hatua hizi
Nenda kwenye ofisi yapolisi wa usalama barabarani ukiwa na leseni yako ya zamani ya udereva kama uliipoteza basi neda hivo hivo na utapewa utaratibu, hakikisha una na umri zaidi ya miaka 18 kwa magari na miaka 16 kwa pikipiki kabla ya kuomba.
KUBADILI LESENI ILI KUPATA YA DARAJA ''C''
Ni muhimu kukumbuka kuwa leseni ya udereva ni hati ya kuthibitisha ujuzi wa kuendesha gari kisheria. Ni jukumu la mmiliki wa leseni kuhakikisha kuwa anafuata sheria na kuendesha gari kwa usalama wakati wote.
Comments