Nakala iliyo pita tuliangalia magari yanayotumia mafuta kidogo, ili iweze kukusaidia kufanya maamuzi sahihi pindi pale unapo taka kununua gari itakayo endana na hali ya uchumi uliyopo. sasa leo pia tunakuletea Orodha ya magari yanayotumia mafuta mengi.
magari haya ni gharama sana kwanzia kwenye bei ya kununua, mafuta, na hata matengenezo pale yanapo pata hitilafu. nitakuelezea Faida na hasara za kumiliki magari ya aina hii hivyo basi chukua kahawa yako au maji kisha soma kwa makini.
Mercedez benz Brabus ni moja katika magari yanoyotumia mafuta mengi sana, kulingana na tovuti yao Gari hii inatumia zaidi ya Lita 13 za mafuta ukitembea kilomita 100. magari haya ni ya kifahari na yanauzwa kwa bei kubwa sana. Mercedez benz brabus mpya inaweza kununuliwa mpaka kwa Tsh Millioni 800.
Aina nyingine ya Magari yanayo tumia mafuta mengi ni Landcruiser v8 Gari hii huuzwa mpaka kwa Tsh Millioni 100 ukiongeza na kodi za TRA, na ujazo wa injini ya gari hii hufikia 5,700cc kama utahitaji kununua aina hii ya gari basi itabidi ujipange.
Landcruiser V8 ni mangari yanayo pendwa sana nchini Tanzania. Hasa viongozi wa serikalini na watu wenye pesa (matajiri) hivyo kablwa hujanunua gari hii ni vizuri ukafahamu kua ina ulaji mkubwa wa mafuta lakini ni gari nzuri sana kwa matumizi ya kusafiria masafa marefu.
Jeep wrangler ni magari yanayo tumia sana katika matumizi ya kijeshi na safari katika barabara za mazingira magumu, Gari hizi hunywa mafuta mengi sana na huuzwa kwa gharama kubwa.
kwa lita 1 ya mafuta Jeep wrangler inatembea kilomita 9 tu, kama huna pesa ya kutosha ya kuihudumia gari utaishia kuinunua na kuipaki kila siku.
Gari aina nyingine ambayo hutumia mafuta yakutosha ni Hummer H2, inasemekana gari hii kwa lita 1 ya mafuta inatembea kilomita 5 tu, Na hio ndio sababu inayo fanya gari hizi zisiwe nzuri kwa watu wanaotafuta magari yanayo tumia mafuta machache.
Hummer H2 ni gharama sana unaweza nunua gari hii mpaka kwa Tsh Milioni 100 ukiweka na kodi. Magari mengine yanayo kula mafuta mengi ni Rolls royce gari hii inahitaji mafuta mengi kwaajili tu ya kutembea mwendo mdogo. Tuangalie faida za kumiliki magari haya.
Faida za kumiliki magari haya
kwanini Baadhi ya Magari yanatumia mafuta mengi?
Magari ya kifahari, yanajulikana kwa uchumi mbaya wa mafuta.hii ni kwasababu magari ya kifahari yana injini kubwa, nzito, zenye nguvu zaidi kuliko za kawaida, ambazo zinahitaji mafuta zaidi ili kuongeza kasi. Pia wana uwiano wa chini wa gear, ambayo pia hufanya gari kuhitaji mafuta zaidi ya kutumia.
asante kwa kusoma Nakala zetu kama utahitaji kununua,kukodisha au kuuza gari yako basi magaribeipoa tupo kukusaidia Kuweka Tangazo lako ni bure kabisa.
Comments