Hakuna mtu asiye bisha kua Toyota IST ni moja katika magari mengi hapa Tanzania, uwingi wa magari haya husababishwa na kuuzwa dukani kwa bei ndogo na uwezo wake wa kutumia mafuta machache.
Engine ya Gari hii ina uwezo wa kubeba kiasi cha Lita za mafuta 40 mpaka 45 hivyo kukufanya uweze kuweka mafuta kidogo na kutembea umbali mrefu bila ya kupata shida ya mafuta yako kuisha.
Toyota IST ina uwezo wa kutembea hadi 12KM ukiweka mafuta ya Lita moja tu.
Gari nyingine pia ambayo husifika kwa kutumia mafuta kidogo ni Toyota Ractis, gari hizi pia huonekana nyingi sana barabarani kwahiyo kama unatafuta gari itakayo kusaidia kuendesha umbali mrefu bila ya kua na mafuta mengi basi moja wapo ni Gari aina ya Ractis.
Tank la mafuta la gari hii lina uwezo wa kubeba mafuta mpaka lita 42, Ractis ni hodari katika kutunza mafuta ukiwa na Lita 1 ya mafuta basi Gari hii inauwezo wa kutembea hadi Kilomita 18.
Ninacho kipendea hasi kwenye Gari hii ni kubwa kiasi ukilinganisha na IST hivyo kuifanya iwe nzuri hata kwa matumizi ya safari za Familia na marafiki.
Moja pia katika gari ambazo huenekana mtaani mara kwa mara ni Gari aina ya passo gari hii ina uwezo wa kutembea kilomita 17 kwa lita moja tu ya mafuta, hivyo maamuzi ni yako tumekuwekea picha pia za gari hizi kuangalia ipi unayo ona inakufaa zaidi.
Toyota RunX ni nzuri sana hasa katika mazingira ya barabara zetu za Africa, gari hii inauwezo wa kusaifiri umbali mrefu. huku Engine ikiendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. nakumbuka nishawahhi kusafiri kutoka mwanza hadi singida kwa kutumia mafuta lita chache tu. Gari hii naifahamu vizuri kwahiyo naongea nikiwa na uzoefu pamoja na ushahidi mkubwa.
uwezo wa gari hii katika kuhifadhi mafuta ina safiri umbali wa kilomita 17 ukiwa na lita 1 ya mafuta. hii huifanya kua sawa na passo. ingawa ukubwa pamoja na vitu vingine gari hizi hutofautiana.
Ukichunguza kwa makini Gari hii kwa ndani Toyota Allex ni gari inayo vutia sana Gari hii ina viti vya ubora, pia Toyota allex inatumia injini za petroli zenye silinda 4 zinazopatikana katika sehemiu mbili, chaguo la 1,496cc ambalo hupakia 110hp na usafirishaji wa 1,795cc na 190hp.
Kwa upande wa matumizi ya mafuta, injini ya mafuta yenye kiwango cha 1.8 hutumia takriban kilomita 12 kwa lita wakati injini ya 1.5L inatumia wastani wa kilomita 15 kwa lita.
Toyota voxy ni gari nzuri inayo kupa nafasi kubwa ya kubeba watu wengi pamoja na mizigo ya ziada.vigezo vingine ni pamoja na uwepo wa runinga ya gari, Airbag, paa la kuzuia mwanga mkali wa jua. Voxy inapatikana kwa wanunuzi kama mifumo ya kuendesha magurudumu ya mbele na ya magurudumu manne, Yaani 4 wheel drive.
Kwa upande wa matumizi ya mafuta, Toyota Voxy hutembea wastani wa kilomita 15.7 kwa Lita.
Toyota Raum ni gari ya aina ndogo Magari haya yanatumia petroli kama magari mengine mengi ambayo tumekwisha yataja hapo awali. Toyota Raum ni Automatic hivyo ni rahisi kuendesha kama ilivyo IST na nyinginezo.
Matumizi ya mafuta hutofautiana kulingana na mfumo uliyopo mfano. Mifumo ya uendeshaji ya FF hutumia wastani wa kilomita 16.2 kwa lita wakati mifumo ya 4WD inatumia kilomita 15 kwa lita. Hivyo Toyota Raum pia ni gari moja wapo ambayo inamatumizi kidogo ya mafuta.
Ikiwa na injini yenye nguvu ya 2,362cc ya petroli inayozalisha 160hp, Ipsum inafanya kazi kikamilifu na inatumia mfumo wa Automatic. Toyota Ipsum ina mifumo miwili ambayo ni 4WD na FF Kama dereva, una chaguo la kuchagua kutoka kwa FF au mfumo wa 4WD.
Kwa hakika, mfumo wa uendeshaji wa FF una kiwango cha matumizi ya mafuta cha 12 km kwa lita wakati mfumo wa gari la 4WD una wastani wa matumizi ya mafuta ya 11 km kwa lita.
Tofauti kati ya 4WD Na FF
Tofauti kuu kati ya FWD na 4WD, ni idadi ya magurudumu (Matairi) ambayo yanaweza kusambaza nguvu. FWD inaweza tu kusambaza nguvu kwa magurudumu ya mbele. Kinyume chake, magari ya 4WD yana uwezo wa kuwasha magurudumu yote manne, ambayo yanaweza kusaidia katika hali fulani.
Toyota vanguard pia ina mfumo wa gari ambayo ni 4WD mfumo huu husaidia matairi yote ya gari kuzunguka, Vanguard pia ni gari ambayo inasifika kwa kua na matumizi madogo ya mafuta japo sio kama magari mengine kama IST ambayo nimekwisha yataja hapo awali.
Matumizi ya mafuta katika gari hii inauwezo wa kutembea hadi 12.6 km kwa lita moja ya mafuta. hii ni kwa injini ndogo ya 2.4L na hutembea kilomita 9.1 kwa lita moja ya mafuta kwenye injini kubwa ya Lita 3.5.
Harrier pia ni gari pendwa sana Tanzania, ikisifika kua na matumizi madogo ya mafuta. Injini ya Toyota Harrier ina uwezo wa kubeba ujazo wa mafuta mpaka Lita 72 na ina uwezo wa kutembea hadi kilomita 11 Kwa lita 1 tu ya mafuta.
Gari hii ni kubwa kiasi na inauwezo wa kutembea umbali mrefu bila kuleta hitilafu yoyote. kama unahitaji gari inayo dumu na yenye matumizi madogo ya mafuta basi Hakikisha Harrier ni moja ya chagua lako.
Magari mengine yenye Matumizi madogo ya Mafuta
Aidha chagua ni lako wewe mwenyewe Tumia nakala hii kuchagua gari ambayo ita kusaidia katika safari zako za kila siku. moja wapo ni matumizi madogo ya mafuta kama utahitaji kununua, kuuza au kukodisha gari ya basi Tovuti yetu ya magaribeipoa ipo kukusaidia kwa hilo.
Comments