Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Aishi Salum Manula mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia mabingwa mara nne wa ligi kuu. Katika mkataba huu mpya, ina semekana thamani yake ni Milioni 300 na kuna ongezeko la thamani kila mwaka.
Kulingana na mkataba huo, Manula atapokea mshahara wa Milioni 8 kila mwezi na thamani ya mkataba wake itaongezeka kwa Milioni 1 kila mwaka. Hii inamaanisha kwamba katika mwaka wa kwanza, mshahara wake utakuwa Milioni 8, katika mwaka wa pili utakuwa Milioni 9 na katika mwaka wa tatu utakuwa Milioni 10.
Mbali na mshahara huo, Manula atapokea pia bonasi mbalimbali kila msimu.
Kwa siku | Tzs 266,667 |
kwa wiki | Tzs 1,800,000 |
kwa mwezi | Tzs 8,000,000 |
kwa mwaka | Tzs 96,000,000 |
Aishi Salum Manula ni mchezaji wa soka kutoka Tanzania ambaye anacheza kama kipa. Alishiriki ligi ya vijana ya Tanzania akiwa na umri wa miaka 14 na baadaye akajiunga na klabu ya Mtibwa Sugar FC. Mwaka 2012, akiwa na umri wa miaka 17, alihamia klabu ya Azam FC. Uwezo wake mkubwa na utulivu katika uchezaji ulimsaidia kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Azam FC, akichukua nafasi ya kipa Daniel Agpeyi kutoka Ghana.
soma pia: Mshahara wa stephane Aziz ki
Mwaka 2017, Manula alihamia klabu ya Simba SC, moja ya klabu kubwa na yenye mafanikio makubwa nchini Tanzania. Alishiriki kwa mafanikio katika kikosi cha Simba SC na kuisaidia klabu hiyo kushinda taji la ligi kuu ya Tanzania na kushinda tuzo ya "Mkono wa Dhahabu" kwa kuwa kipa bora wa ligi hiyo. Manula amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi cha Simba SC na pia amewahi kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Kwa mafanikio yake makubwa na uwezo wake mkubwa, Manula amekuwa mmoja wa makipa bora nchini Tanzania. Ameongoza Simba SC kushinda taji la ligi kuu ya Tanzania mara nne mfululizo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021. Pia, amesaidia klabu hiyo kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kama vile Ligi ya Mabingwa Afrika.
kwa maoni au swali lolote kuhusu mshahara wa mchezaji Aishi salum manula unaweza kuandikia kupitia sehemu ya comment hapo chini
Comments