Je ungependa kufahamu ulaji wa mafuta wa Gari aina ya Toyota Premio, inawezekana ungependa kununua au Tayari umekwisha inunua gari hii na bado Hujafahamu matumizi ya mafuta ya gari yako basi leo nitakujuza.
kwani itakusaidia kujua ni fedha kiasi gani utahitaji kutumia katika Gari yako hasa kwenye suala zima la mafuta kulingana na mwendo utakao safiri. Katika nakala hii nitakueleza kila kitu unachopaswa kujua kuhusu Matumizi ya mafuta ya Toyota Premio.
Toyota hajawahi kufeli hasa katika kutengeneza magari yasiyo Tumia mafuta mengi, Premio ni Gari nzuri sana hasa linapokuja swala la matumizi ya mafuta, gari hii hutumia mafuta kidogo tu na huenda mwendo mrefu ukilinganisha na magari mengine.
Toyota Premio inatumia Petrol na hutembea wastani wa umbali wa Kilomita 15 hadi 20 kwa lita 1 tu ya mafuta.
Lakini sio kwamba Premio zote zina matumizi sawa ya mafuta angalia cc ya injini yako kwani zipo za 1501cc mpaka 2000 CC, kwahio matumizi niliyo kuwekea hapo ni makadirio ila inaweza ikawa tofauti kidogo.
Aina hii ya gari injini yake ina ujazo mdogo wa wastani wa 1501CC sawa na Lita 1.5 hivyo kuweza kuchukua kiasi kidogo tu cha mafuta, pia Gari hii haina matumizi mengi ya mafuta ukilinganisha na gari zingine za kifahari zinazo tumia mifumo Tofauti hivyo kuhitaji mafuta ya ziada katika kusukuma gari hilo.
Hivyo basi kama nilivyosema hapo awali kama utahitaji gari kwaajili ya safari ndogo ndogo, nasio za kusafiri masafa marefu basi Premio ni gari nzuri, ila kama utahitaji gari za kufanyia safari za mbali gari hii inaweza isiwe chaguo sahihi kwako. kwani kwajinisi ilivyo tengenezwa gari hii haiweza kustahmili safari ndefu ukilinganisha na magari kama Landcruiser V8 na mengineyo.
Nazani mpaka sasa umesha fahamu swala zima la matumizi ya mafuta katika gari ya Toyota Premio kama utakua na swali lolote unaweza kuweka comment yako hatpo chini nasi tutakujibu
Soma pia Toyota Harrier ulaji wa mafuta
Comments