Inawezekana unahitahi gari kwa ajili ya matumizi mbalimbali hivyo basi gharama ya gari hutofautiana kulingana na ubora, matumizi na kampuni ya kutengeneza gari hio. Mfano kampuni ya Toyota hutofautiana bei na kampuni ya kutengeneza magari ya Mercedez benz kwa sababu mbalimbali moja wapo ni ubora.
Sasa bila kupoteza muda nimezigawa Aina za magari katika sehemu kuu tatu nayo ni:-
Gari ndogo hii hujumuisha magari kama Toyota IST, vitz, corolla na gari zenye muundo wa Tax. gari hizi ni nzuri kwa safari zisizo hitaji kusafiri umbali mrefu maranyingi hutumika kama chombo cha usafiri (uber na bolt)
Hii ni Aina za gari zenye bei ndogo sana, na hupatikana kwa wingi wastani wa bei wa magari haya ni TSH 10M-25M ikiwa mpya.
Gari hizi zinasifa ya kutumia mafuta kidogo hivyo huokoa muda na fedha ambao ungeutumia kupanga foleni sheli ingawa magari haya sio imara.
Gari hizi huitwa SUV yaani sport utility vehicles Magari haya ni mazuri kwa safari zenye umbali mrefu na mfano wa gari hizi ni kama Toyota Landcruiser Hardtop, ALPHARD, V8, Range rover na NK, magari haya ni gharama sana.
magari haya husifika kwa kua na nguvu ya injini na kunywa Mafuta mengi. kama utahitaji gari kwa ajili ya safari zako kwenda mikoa mbali mbali na familia basi ,Gari za aina hii zitakufaa sana.
Wastani wa bei za magari haya ni TSH 30M-200M zikiwa mpya
mfano Gari kama V8 huuzwa zaidi ya Tsh 100M, hhivyo basi magari haya maranyingi haya tumiki katika biashara bali matumizi ya kiserikali na binafsi.
Hii aina ya magari hujumuisha magari kama lory, mabasi, na kadhalika magari haya maranyingi hutumika kwaajili ya bishara na huuzwa kwa bei kubwa sana, ina injini zenye ujazo mkubwa kwahiyo hata utumiaji wake wa mafuta hua ni mkubwa zaidi.
magari haya ni kama scania, mabasi ya yutong, fuso na mengineyo.
wastani wa bei za magari haya ni TSH 100M- 200M ikiwa mpya
hivyo basi aina za gari utakayo taka kuinunua pia hutegemea na matumizi yako. niambie kwenye comment section hapo chini ni aina ipi ya Gari unaikubali nami nitakujibu kwa haraka pia kama una uza au unahitaji kununa magari kwa bei poa tembelea tovuti yetu na uweke tangazo lako bure.
Aina hizi za magari tulizokuwekea ni za bei tofauti tofauti, hivyo basi ni wewe utachagua unayo ona inakufaa zaidi pia, kama umependezwa na nakala hii basi tuambie kwenye comment hapo chini.
Comments