Je ungependa kufahamu ulaji wa mafuta wa Gari aina ya Toyota IST, inawezekana ungependa kununua au Tayari umekwisha inunua gari hii na bado Hujafahamu matumizi ya mafuta ya gari yako basi leo nitakujuza.
kwani itakusaidia kujua ni fedha kiasi gani utahitaji kutumia katika Gari yako hasa kwenye suala zima la mafuta kulingana na mwendo utakao safiri. Katika nakala hii nitakueleza kila kitu unachopaswa kujua kuhusu Matumizi ya mafuta ya Toyota IST.
IST ni Gari nzuri sana hasa linapokuja swala la matumizi ya mafuta, gari hii hutumia mafuta kidogo tu na huenda mwendo mrefu ukilinganisha na magari mengine.
Toyota IST inatumia Petrol na hutembea wastani wa umbali wa Kilomita 12 kwa lita 1 tu ya mafuta.
Bei ya petrol mpaka sasa ninavyo andika Nakala hii ni wastani wa Tsh 3000 Kwa lita, hivyo basi Kama utahitaji gari itayo kusaidia katika swala zima la uchumi wa mafuta basi moja ya gari za kununua ni IST.
Aina hii ya gari injini yake ina ujazo mdogo wa wastani wa 1500CC sawa na Lita 1.5 hivyo kuweza kuchukua kiasi kidogo tu cha mafuta, pia Gari hii haina matumizi mengi ya mafuta ukilinganisha na gari zingine za kifahari zinazo tumia mifumo Tofauti hivyo kuhitaji mafuta ya ziada katika kusukuma gari hilo.
Hivyo basi kama nilivyosema hapo awali kama utahitaji gari kwaajili ya safari ndogo ndogo, nasio za kusafiri masafa marefu basi IST ni gari nzuri, ila kama utahitaji gari za kufanyia safari za mbali gari hii inaweza isiwe chaguo sahihi kwako. kwani kwajinisi ilivyo tengenezwa gari hii haiweza kustahmili safari ndefu ukilinganisha na magari kama Landcruiser V8 na mengineyo.
Nazani mpaka sasa umesha fahamu swala zima la matumizi ya mafuta katika gari ya Toyota IST kama utakua na swali lolote unaweza kuweka comment yako hatpo chini nasi tutakujibu.
Soma pia: Toyota spacio ulaji wa mafuta Fahamu zaidi
Comments