Je ungependa kufahamu ulaji wa mafuta wa Gari aina ya Toyota corolla spacio, inawezekana ungependa kununua au Tayari umekwisha inunua gari hii na bado Haujafahamu matumizi ya mafuta ya gari yako basi leo nitakujuza.
Hii itakusaidia kujua ni fedha kiasi gani utahitaji kutumia katika Gari yako hasa kwenye suala zima la mafuta kulingana na mwendo utakao safiri. Katika nakala hii nitakueleza kila kitu unachopaswa kujua kuhusu Matumizi ya mafuta ya Toyota spacio.
Spacio ni Gari nzuri sana hasa linapokuja swala zima la matumizi ya mafuta, gari hii hutumia Mafuta kidogo tu na huenda mwendo mrefu ukilinganisha na magari mengine
Toyota spacio inatumia Petrol na hutembea wastani wa umbali wa Kilomita 10 kwa lita 1 tu ya mafuta. hivyo basi ulaji wa mafuta kwa spacio hautofautiani sana na ule wa Toyota IST Bofya link hapo kusoma.
Bei ya petroli mpaka sasa ninavyo andika Nakala hii ni wastani wa Tsh 3000 Kwa lita, hivyo basi Kama utahitaji gari itayo kusaidia katika swala zima la uchumi wa mafuta basi moja ya gari za kununua ni Toyota spacio.
Make: | TOYOTA |
Model | COROLLA SPACIO |
Body Type | HATCHBACK |
year of manufacture | 2003 |
country | JAPAN |
Engine capacity | 1501-2000cc |
Fuel type | petrol |
Aina hii ya gari injini yake ina ujazo mdogo wa wastani wa 2000CC sawa na Lita 1.5 hivyo kuweza kuchukua kiasi kidogo tu cha mafuta, pia Gari hii haina matumizi mengi ya mafuta ukilinganisha na gari zingine za kifahari zinazo tumia mifumo Tofauti hivyo kuhitaji mafuta ya ziada ili kusukuma gari hilo.
Hivyo basi kama nilivyosema hapo awali kama utahitaji gari kwaajili ya safari ndogo ndogo, nasio za kusafiri masafa marefu basi Spacio ni gari nzuri, ila kama utahitaji gari za kufanyia safari za mbali gari hii inaweza isiwe chaguo sahihi kwako. kwani kwajinisi ilivyo tengenezwa gari hii haiweza kustahmili safari ndefu ukilinganisha na magari kama Landcruiser V8 na mengineyo.
Nazani mpaka sasa umesha fahamu swala zima la matumizi/ulaji ya mafuta katika gari ya Toyota Spacio kama utakua na swali lolote unaweza kuweka comment yako hapo chini nasi tutakujibu.
Comments