Mshahara wa askari magereza ni kati ya Tsh 400,000 hadi Tsh 600,000 Na hulipwa kulingana na vyeo
Askari magereza ni watumishi wa serikali ambao wanafanya kazi katika magereza kusimamia na kutekeleza majukumu yote yanayohusiana na utawala wa gereza na usalama wa wafungwa. Majukumu yao yanaweza kujumuisha kulinda usalama na amani ya magereza, kusimamia shughuli za wafungwa, kuhakikisha utaratibu wa magereza unafuatwa, kusimamia mpango wa lishe ya wafungwa, kutoa huduma za afya kwa wafungwa na kusimamia vifaa vya magereza. Pia, wanaweza kushiriki katika kazi za uchunguzi wa uhalifu ndani na nje ya magereza.
Fahamu kua mishahara ya askari polisi ina tofautiana na wa magereza kuanzia ufanyaji kazi, mafunzo pamoja na vitu vingine vingi tu.
ili uwe askari magereza na uanze kulipwa mshahara unahitaji kupatiwa mafunzo na baada ya kufaulu askari magereza hupata mafunzo maalum ya kijeshi na kitaalamu ili kuwawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi na uadilifu. Mafunzo haya yanajumuisha mafunzo ya kijeshi, sheria na taratibu za magereza, utaratibu wa utawala wa magereza, utunzaji wa wafungwa, ulinzi na usalama, mafunzo ya kujikinga na kuzuia magonjwa, mafunzo ya kutoa huduma ya kwanza, na mafunzo ya maadili na utawala bora.
Mafunzo haya hutolewa na Chuo cha Magereza Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania (Tanzania Prisons Service). Baada ya mafunzo hayo, askari magereza huwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kufanya kazi yao kwa ufanisi na uadilifu, na wanakuwa tayari kuanza kazi katika magereza yoyote nchini Tanzania.
soma pia:-
Mshahara wa stephane aziz ki wa yanga
Comments